Siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 7 juni.

Siku kama hii ya leo miaka 139 iliyopita, sawa na tarehe 7 Juni 1879 vilianza vita vilivyochukua muda wa miaka mitano kati ya nchi za Peru, Chile na Bolivia. Vita hivyo vilianza baada ya serikali ya Bolivia kutiliana saini na shirika moja la Chile na kisha kukiuka makubaliano ya mkataba huo, na kusababisha Chile kuishambulia kijeshi Bolivia. Hatimaye Chile ilijipatia ushindi kwenye vita hivyo, na kutiliana saini makubaliano mapya na nchi za Bolivia na Peru, ambapo kwa mujibu wa makubaliano hayo, ufukwe wote wa Bolivia na sehemu ndogo ya ardhi ya Peru ilichukuliwa na Chile.

Na Siku kama hii ya leo miaka 170 iliyopita, sawa na tarehe 7 Juni mwaka 1848 alizaliwa Paul Gauguin mchoraji mashuhuri wa Kifaransa. Gauguin alizaliwa Ufaransa na kisha kumuoa mwalimu aliyekuwa mahiri katika fani ya uchoraji, na kusababisha Gauguin kuvutiwa na sanaa hiyo iliyomuwezesha kuacha athari zake za sanaa ya uchoraji katika kisiwa cha Tahiti, kilichoko kusini mwa Bahari ya Pacific. Gauguin aliishi kwenye kisiwa hicho hadi mwisho wa umri wake mwaka 1903, kwa kuchora picha zinazoakisi mandhari mbalimbali.

Siku kama ya leo miaka 175 iliyopita, alifariki dunia Johann Friedrich Hölderlin, malenga mkubwa wa nchini Ujerumani. Alizaliwa tarehe 20 Machi 1770 katika familia masikini ambapo akiwa kijana mdogo alifiwa na baba yake mzazi. Friedrich Hölderlin pia alijifunza elimu ya dini katika chuo kikuu ambapo alitokea kuwa na hisia za utumishi na urafiki sambamba na kusoma mashairi ya kidini. Malengo ya kupigania uhuru ya Ufaransa ni mambo yaliyotawala fikra za Johann Friedrich Hölderlin. Hata hivyo licha ya kwamba alikuwa na harakati mbalimbali lakini athari zake muhimu hazikuonekana kwa kipindi cha miaka 100 tangu kufariki kwake dunia. Miongoni mwa athari za Johann Friedrich Hölderlin ni ‘Sherehe ya amani’ na ‘Mashairi ya Usiku’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

×

Like us on Facebook