Diamond, Nandy, Mpoto na Monalisa Watinga Bungeni

Wanamuziki Diamond, Nandy na Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba ni miongoni mwa wageni waliohudhuria kikao cha Bunge leo,  Aprili 27,  mjini Dodoma.
Wanamuziki hao pamoja na Lipumba walishangiliwa na wabunge baada ya kutambulishwa na mwenyekiti wa Bunge, Musa Azzan Zungu.
Mbali na wasanii hao na Lipumba, wengine waliotambuliwa ni mwanamuziki Mrisho Mpoto na msanii wa filamu Monalisa.
Zungu amesema wote ni wageni wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo. Bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 inasomwa leo.


Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *