Siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 26 April.

JE WAJUA? kuwa muda mrefu zaidi kwa binaadamu aliyekaa kwenye ”coma” yaani mahututi asiyejitambua ni miaka 37?

Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita yaani mwaka 1964 kulitokea utiaji saini wa muungano wa visiwa vya unguja na pemba dhidi ya Tanganyika,ambapo ilikuja kuzaa jina la muunganiko huo ulioitwa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Siku kama ya leo mwaka 1938 mji wa Basque unaopatika huko Guernica kaskazini mwa uhispania waangamizwa na ndege washirika za ujerumani zilizokuwa zinamsaidia kiongozi wa wakati huo bwana Franco katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Na vilevile siku kama ya leo mwaka 1986 mlipuko uliotokea katika kinu cha nyuklia huko katika mji wa Chernobyl,Ukraine wasababisha maafa makubwa kabisa katika historia ya nyuklia duniani.

Na siku kama ya leo mwaka 1929 safari ya ndege ya moja kwa moja kati ya Uingereza na India yamalizika

Siku kama ya leo mwaka 1514 sayari ya Saturn iligunduliwa kwa mara ya kwanza na bwana CopernicusAuthor: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *