Siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 15 April.

Siku kama ya leo miaka 566 iliyopita, alizaliwa mchoraji na msanii mashuhuri wa kutengeneza vinyago wa Italia Leonardo da Vinci. Mwaka 1461 alianzisha kituo cha uchoraji katika mji wa Florence nchini Italia na hatua kwa hatua akaanza kupata umashuhuri katika uchoraji. Alionesha kipaji kikubwa cha kuchora akiwa bado mtoto mdogo na alikweya daraja za juu katika fani hiyo haraka mno. Mwaka 1506 da Vinci alichaguliwa kuwa mchoraji wa Mfalme Luis wa 12 kisha akawa mchoraji wa Mfalme Francis wa Kwanza.

Picha inayohusianaMchoro wa yesu na wafuasi wake uliochorwa na Leonardo da Vinci

Mbali na uhodari wake katika kuchora na kutengeneza vinyago, Leonardo da Vinci pia alisomea fizikia na hisabati. Miongoni mwa kazi zake mashuhuri ni michoro ya kanisa kuu la mji wa Milan, mchoro wa picha ya “Tabasamu la Jugund,” picha ya Mona Lisa na ya Karamu ya Mwisho ya sanamu la Yesu ama nabii Issa Masih. Leonardo da Vinci alifariki dunia mwaka 1519 akiwa na umri wa miaka 67.

Siku kama ya leo miaka 106 iliyopita meli kubwa ya abiria ya Titanic ambayo ilitambuliwa kuwa nembo ya mafanikio makubwa ya viwanda vya meli vya wakati huo yazama kabisa baharini baada ya kugonga mwamba wa theluji katika Bahari ya Atlantic, katika safari yake ya kwanza kutoka bandari ya Southampon nchini Uingereza kuelekea New York, Marekani. Zama hizo Titanic ilitambuliwa kuwa meli kubwa zaidi na ya kifahari kuliko meli nyingine zote duniani. Watengenezaji wa meli hiyo walikuwa wakisema kuwa haingeweza kuharibika na kuzama. Ni wasafiri 705 tu kati ya abiria wake wote 2207 waliokuwemo kwenye meli hiyo ndio waliookoka katika ajali hiyo. Ajali hiyo inatambuliwa kuwa ajali mbaya zaidi ya baharini na iliyosababisha idadi kubwa ya vifo vya watu duniani.

Na siku kama ya leo miaka 24 iliyopita, ulitiwa saini mkataba wa kuanzisha Shirika la Biashara Duniani (WTO) nchini Morocco. Utangulizi wa kuasisiwa shirika hilo ulifanywa na Marekani na Uingereza wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na kwa msingi huo, mwaka 1947 nchi 23 zilizoendelea zilitia saini makubaliano ya kuanzisha GATT. Makubaliano hayo yalisisitiza juu ya kufanyika mazungumzo ya kupunguza ushuru wa forodha, vipingamizi vya biashara na kuondoa vizuizi vya biashara huru. Baadaye jumuiya ya GATT ilibadilishwa jina na kuwa WTO na hati yake ilianza kutekelezwa Januari mwaka 1995. Hata hivyo Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimeliteka nyara shirika hilo la kibiashara duniani na kulitumia kwa faida na maslahi yao wenyewe.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *