Mwanamke wa Kwanza Kupata shahada Tanzania Atunukiwa Tuzo.

KAMA ulikuwa hufahamu basi naomba hii uiweke kwenye ubongo wako, Dkt Maria Kamm ndiye mwanamke wa kwanza wa Tanzania kupata Shahada ya kwanza (Degree) na leo ametunukiwa tuzo ya heshima katika tuzo za Malkia wa Nguvu zinazoandaliwa na Clouds Media.

Mama Kamm ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Weruweru iliyopo Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, akiwa kama Mzalendo wa kweli, ametumia maisha yake kwa kiasi kikubwa kuwashauri na kuwaelimisha vijana katika masuala mbalimbali ya Taifa.

Mgeni Rasmi katika utoaji wa Tuzo hizo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwl Nyerere Posta jijini Dar, alikuwa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, dkt. ummy Ally Mwalimu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *