Siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 13 March.

JE WAJUA? kwa kawaida paka yoyote mweupe mwenye macho ya blue ni kiziwi? na je wajua? ukuta mkubwa wa huko china unakadiriwa kuwa na urefu wa kilometa 6,430 sawa na kutoka dar es salaam mpaka arusha mara 10?

……………………………………………………………………………………………………………………………………….

Siku kama ya leo miaka 285 iliyopita, yaani 13 Machi, 1733 alizaliwa Joseph Priestley, mwanakemia na mwanafizikia wa Uingereza. Msomi huyo aliishi katika kipindi kilichokuwa maarufu kama zama za dhahabu za kemia. Katika uchunguzi na utafiti wake, Priestley alivumbua uvutaji pumzi katika mimea kwa gesi za oksijeni na haidrojeni. Joseph Priestley alifariki dunia mwaka 1804.

Siku kama ya leo mwaka 1781 mtaalamu wa mambo ya anga yaani unajimu mwingereza Frederick William Herschel aigundua sayari ya Uranus

Siku kama ya leo miaka 70 iliyopita sawa na tarahe 13 Machi 1948, Waisrael waliokuwa na mfungamano na kundi la kigaidi la Haganah, walishambulia kitongoji cha Wapalestina cha Husseiniyah katika eneo la kaskazini mwa Jalilah. Waisrael hao licha ya kuwaua zaidi ya Wapalestina 60, waliharibu nyumba zao kadhaa. Hali kadhalika katika siku hiyohiyo, wanajeshi wa Israel walizilipua kwa mabomu nyumba za Wapalestina katika eneo la ‘Qatmuun’ lililoko Baitul Muqaddas. Mauaji ya Palestina yaliyofanywa na makundi ya kigaidi ya Israel, yalitekelezwa kwa lengo la kutaka kutangaza uwepo wa utawala huo kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina baada ya kuondoka vikosi vya Uingereza katika eneo hilo.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *