Mahusiano ya Alikiba na mrembo wa Kenya yaanza kuvuja.

Kamera zinazidi kummulika Alikiba. Ukweli wa mahusiano yake na mrembo kutoka mjini Mombasa, Kenya anayefahamika kama Aminah umeanza kufichuka wazi.

mrembo huyo ambao kwa mujibu wa vyanzo vyetu kutoka Kenya vilituambia kuwa walitakiwa kufunga ndoa Machi 2 ya mwaka huu, hata hivyo stori kamili kilichoendelea kuhusu ndoa hiyo hatukuweza kuzipata.

Hata hivyo ukweli wa mahusiano ya wawili hao umeanza kuonekana wazi kutokana na moja ya ujumbe huo hapo juu ambao Alikiba na Aminah walitumiana kupitia mtandao wa Twitter. Kupitia mtandao huo Aminah anatumia jina la AmyRekish.

 

Kwa mujibu a vyanzo vyetu vimeendelea kumtafuta mrembo huyo na kupata taarifa kuwa anafanya kazi ya Fiscal analyst (Mchambuzi wa fedha) kwenye serikali ya kaunti ya Mombasa.

Chanzo hiko kimeendelea kwa kusema kuwa Alikiba na Aminah wameanza mahusiano tangu mwaka 2016 na pia inadaiwa kuwa mrembo huyo ndiye aliyempokonya tonge mdomoni mrembo Jokate Mwegelo ambaye mara kadhaa aliwahi kudaiwa kuwa na mahusiano ya msanii huyo.

Picha ya Aminah ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wa Alikiba

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *