Kenyatta, Odinga Kufanya Ziara ya Kuzunguka Nchi Nzima.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na hasimu wake ambaye ni kiongozi wa umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, Raila Odinga wamepanga kufanya ziara ya nchi nzima kuhamasisha amani, mshikamano na umoja.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star limeripoti kuwa ziara hiyo itaanzia maeneo ambayo vyama vya upinzani nchini humo vina nguvu zaidi na kuendelea maeneo mengine.

Gazeti hilo limeripoti kuwa ziara hiyo itaanzia jimbo la Nyanza ingawaje tarehe rasmi ya ziara hiyo bado haijatangazwa.

Wakati hayo yakijiri, viongozi wa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya leo Jumatatu wanatarajia kuongea na waandishi wa habari kuhusu mustakabari na muelekeo wa umoja huo.

Wiki iliyopita Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga alikutana na Rais Uhuru Kenyatta kwenye Ikulu ya nchi hiyo ambapo kwa pamoja walikubaliana kujenga nchi na kuweka mbali tofauti zao za kisiasa.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *