Siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 11 March.

JE WAJUA? kwa wastani mtu wa makamo hutumia jumla ya miaka 25 kwenye kulala tu? na je wajua? kuna sekunde 31,557,600 katika mwaka mmoja?

Siku kama ya leo miaka 15 iliyopita yaani mwaka 2004, kufuatia miripuko 10 ya mabomu kwenye vituo kadhaa vya treni ya chini ya ardhi (Metro) mjini Madrid Uhispania, watu karibu 200 waliuliwa na wengine 18,000 kujeruhiwa. Miripuko hiyo inahesabiwa kuwa ni miongoni mwa vitendo vikubwa vya kigaidi kuwahi kutokea Uhispania na Ulaya tangu mwishoni mwa vita vya Pili vya Dunia. Baada ya kutokea miripuko hiyo serikali ya wakati huo nchini humo iliituhumu kundi la Eta Basque ambalo linadai kujitenga na utawala wa nchi hiyo, kwamba ndilo lililohusika na miripuko, hata hivyo kundi la Al Qaida lilitangaza kuhusika katika miripuko hiyo. Miripuko hiyo ya Machi 11 ilitokea wakati chama cha Socialist kikiwa kimeshinda katika uchaguzi wa Bunge nchini humo na kuondoka vikosi vya Uhispania nchini Iraq.

Miaka 8 uliopita katika siku kama ya leo yaani machi 11 mwaka 2011, tetemeko la ardhi lililokuwa na ukubwa daraja 9 kwa kipimo cha richta lililikumba eneo la Tohoku lililopo mkoa wa Miyagi Mashariki mwa Japan. Tetemeko hilo lilipelekea kuuawa kwa watu elfu 12 na malaki kadhaa ya wengine kubakia bila makazi kufuatia tetemeko hilo ambalo halijawahi kutokea mfano wake tangu makumi ya miaka yaliyopita nchini humo. Tetemeko hilo lilibomoa miundombinu, makazi ya raia na taasisi mbalimbali na kuiletea hasara ya mabilioni ya pesa nchi hiyo, kiasi kwamba kwa muda kadhaa Japan ilikuwa katika hali mbaya ya kiuchumi. Tetemeko hilo lilizua mawimbi ya Tsunami yaliyokuwa na mwinuko wa mita 15, huku mawimbi mengine madogo madogo yakizikumba nchi nyingine za jirani kufuatia tetemeko hilo.

Tarehe 11 Machi mwaka 2006 dikteta wa zamani wa Yugoslavia Slobodan Milosevic akiwa na umri wa miaka 64 alifariki dunia ndani ya jela katika mji wa the Hague. Miezi 9 baada ya kuanguka utawala wake mwaka 2001, Milosevic alitiwa mbaroni na kukabidhiwa na Yugoslavia ya zamani, kwenye mahakama ya uhalifu wa kivita ya mjini the Hague. Akiwa kijana alijiunga na chama cha Ucomonist cha Yugoslavia ya zamani. Mwaka 1989 Milosevic akawa Rais wa Serbiya. Milosevic aliongoza vita vilivyoanza mwaka 1992 vilivyo dumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Katika vita hivyo waislamu wa Bosnia laki mbili waliuawa, huku wengine milioni 2 wakibakia kuwa wakimbizi. Kufuatia kushindwa kwa Slobodan katika uchaguzi mwaka 2000 na kushadidi upinzani wa ndani dhidi yake, hatimaye utawala wake ulianguka na baada ya muda kidogo akatiwa mbaroni. Kesi ya Milosevic ilianza kusikilizwa mwaka 2002, hata hivyo kifo chake kilitokea kabla ya kumalizika kesi hiyo.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *