katika historia March 10-Simu ya kwanza duniani ilivumbuliwa na kujaribiwa na Alexander Graham Bell

Tarehe 10 Machi miaka 142 iliyopita mvumbuzi wa Kimarekani Alexander Graham Bell alivumbua simu na siku hiyo hiyo akafanya mazungumzo ya kwanza ya majaribio ya simu na msaidizi wake Thomas Watson. Uvumbuzi huo wa simu ulileta mabadiliko makubwa katika vyombo vya mawasiliano.Bell alifaidika na uzoefu na majaribio ya wahakiki na wavumbizi wengine katika kutengeneza chombo hicho cha mawasiliano ya haraka. Baada ya hapo chombo cha simu kiliboreshwa na kufikia kiwango cha sasa kwa kukamilishwa kazi iliyofanywa na Alexander Graham Bell.

Tarehe 10 Machi siku kama ya leo miaka 121 iliyopita jeshi la Italia lilishindwa vibaya katika jaribio lake la kutaka kuivamia na kuikalia kwa amabavu Uhabeshi au Ethiopia ya sasa. Lengo kuu la shambulizi hilo la Italia lilikuwa ni kuiungunisha Ethiopia na makoloni mengine mawili ya nchi hiyo yaani Somalia na Eritrea. Katika vita hivyo jeshi la Italia lilipata kipigo na hasara kubwa ya hali na mali licha ya kuwa na silaha za kisasa na kulazimika kurudi nyuma.

Siku kama ya leo miaka 72 iliyopita wakati wa Vita vya Pili vya Dunia ndege za kivita za Marekani zilifanya mashambulizi makubwa dhidi ya mji mkuu wa Japan, Tokyo. Mashambulizi hayo makubwa yalishirikisha mamia ya ndege kubwa za kurusha mabomu za Marekani zilizomimina mabomu kwa mara kadhaa katika mji mkuu wa Japan. Karibu raia laki moja wa nchi hiyo waliuawa katika mashambulizi hayo.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *