Alichokisema Papi kocha baada ya nyimbo za Diamond na Nay kufungiwa.

Wakati mjadala ukiendelea baada ya sekali kufungia baadhi ya nyimbo za wasanii ambazo zilionekana kwenda kinyume na maadili, Papii Kocha ametoa mtazamo wake kuhusuana na hilo.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Waambie’ ameunga mkono hatua hiyo na kusema kuwa msanii anapaswa kutunga muziki wenye kuelimisha.

“Msanii anatakiwa awe anaelimisha jamii sasa ukiandika vitu ambavyo vipo kinyume utakuwa unaharibu taifa na mataifa mengine ambayo yanapenda kusikiliza muziki wako,” Papii ameiambia Clouds.

February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari. Katika list hiyo Nay wa Mitego alifungiwa nyimbo tatu na Diamond nyimbo mbili.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *