katika historia march 8 – Alizaliwa mwanaanga Yuri Gagarin binaadamu kwa kwanza kutoka nje ya dunia.

JE WAJUA? kuwa ulimi ndio sehemu rahisi kupona zaidi kwenye mwili wa binaadamu? na je wajua? mdudu Kerengende ”dragonfly” ama jina maarufu ”chande” ana miguu 6 lakini haitembei?

………………………………………………………………………………………………………………………….

Siku kama ya leo miaka 84 iliyopita yaani kwani 1934 alizaliwa mwanaanga wa kirusi bwana Yuri Gagarin ambaye ni binaadamu wa kwanza kutoka nje ya dunia.

Na siku kama ya leo mwaka 1959 mdoli wa kike wa kuonyesha mitindo na urembo almaarufu kwa jina la ”BARBIE’ wazinduliwa huko New York Marekani’

Na siku kama ya leo mwaka 1945 ndege za kijeshi za Marekani zilifanya mashambulizi mabaya dhidi ya japani na kuua takribani watu 250,000.

Miaka 564 iliyopita sawa na tarehe 9 mwezi Machi mwaka 1454 alizaliwa mvumbuzi na baharia wa Kiitalia kwa jina la Americo Vespucci. Vespucci alijishughulisha na kazi za melini kutokana na hamu yake kubwa ya kupenda ubaharia aliyoionyesha tangu akiwa kijana na hivyo kupewa cheo cha unahodha. Baharia Americo Vespucci alisafiri mara nne katika nchi isiyojulikana ambayo hadi wakati huo ilikuwa haina jina na baadaye ikapatiwa jina la mvumbuzi huyo wa Kiitalia yaani Amerika.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *