Siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 10 Februari.

Siku kama ya leo mwaka 1906 Jeshi la majini la uingereza Royal Navy lazindua meli kubwa ya kivita ya kwanza dunia ambayo ilijulikana kama ”Dreadnought”

Siku kama ya leo miaka 255 iliyopita kulitiwa saini mkataba baina ya Uingereza na Ufaransa huko katika mji wa Paris. Wafaransa waliutaja mkataba huo kuwa mbaya sana. Hii ni kutokana na kuwa, kwa mujibu wa mkataba huo, baada ya miaka mingi ya vita na mivutano na Uingereza, Ufaransa ilikubali kufumbia macho madai yake yote na maslahi yake ya kikoloni huko India na Canada. Sababu ya kutiwa saini mkataba huo ni kwamba, katika zama hizo Ufaransa ilikuwa imedhoofika kutokana na kujihusisha na vita mbalimbali barani Ulaya na kwa upande wa kijeshi na kiuchumi haikuwa na ubavu wa kuendelea kupigana vita na Uingereza.

Siku kama ya leo miaka 68 iliyopita yaani tarehe 10 Februari mwaka 1950, Joseph Mc Carthy Seneta wa chama cha Republican cha nchini Marekani aliwasilisha orodha ya majina ya wafanyakazi 205 wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo akiwatuhumu kuunga mkono ukomonisti na kuifanyia ujasusi Urusi ya zamani. Hatua hiyo ilipelekea kuanza kwa kile kilichojulikana kama “Mc Carthisim” huko nchini Marekani, ambapo kwa mujibu wake wanafikra, wataalamu na viongozi mbalimbali wa Marekani walifuatiliwa nyendo zao na kusakwa baada ya kutuhumiwa kuwa na mitazamo na fikra za Kikomonisti na kuifanyia ujasusi Urusi ya zamani. Kamisheni ya Mc Carthisim ambayo ilikabiliwa na upinzani mkubwa, iliweza kuwafuta kazi karibu watumishi wa serikali wapatao 2000 huku idadi kubwa ya wataalamu na wasomi wakiswekwa jela kwa tuhuma zisizokuwa na msingi.

Na siku kama ya leo miaka 71 iliyopita, tawala za waitifaki na zile zilizokuwa zikihasimiana katika Vita vya Pili vya Dunia zilisaini makubaliano ya amani. Katika siku hiyo, Marekani, Urusi ya zamani, Uingereza na Ufaransa zilisaini makubaliano ya amani na nchi zilizoshindwa katika vita hivyo yaani Italia, Finland, Poland, Hungary, Romania na Bulgaria, na kwa utaratibu huo nchi sita hizo kwa mara nyingine tena zikajipatia uhuru wake.

JE WAJUA? Ndizi unazokula zina aina flani ya mionzi? lakini ondoa shaka kwa hesabu za wanasayansi mionzi hiyo itaweza kuua iwapo utaweza kula ndizi millioni 10 kwa siku ambapo kamwe haiwezi kutokea.Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *