Breaking News: Mzee Kingunge Ngombale Mwiru afariki dunia.

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Mzee Kingunge Ngombale-mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospital ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu

Mtoto wa marehemu aitwaye Tonny Ngombale-Mwiru amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake.

Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.

Mapema mwanzoni mwa mwezi Januari, mke wa Kingunge Peres Kingunge alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kupooza.

Taarifa zaidi kuhusu msiba na mazishi tutaendelea kukujulisha, endelea kuwa nasi.

Mzee Kingunge alizaliwa Mei 30 mwaka 1930, amefariki akiwa ana umri wa miaka ipatayao  87.

Mzee Kingunge  alikuwa kada aliyekulia ndani ya chama tawala cha CCM , lakini mnamo mwaka 2015 alitangaza kukihama hicho na kwenda kujiunga chama cha CHADEMA akiunga mabadiliko na hivyo amefariki akiwa ni mwanachama wa CHADEMA

Image result for Kingunge Ngombale Mwiru

Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru akihudumu kama Mkuu wa Mkoa wa Singida mwaka 1971.

 Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *