Mbwana Samatta atangaza habari njema.

Baada ya watanzania na mashabiki wa soka watanzania wakiwa wanasononeka kutokana na kipenzi chao na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta kusikia kuwa ameumia goti na kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili alipoumia akiwa na timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Jana January 6 2017 Mbwana Samatta amewatangazia watanzania habari njema, Samatta amewajulisha mashabiki wake na watanzania kuwa baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili sasa amerudi uwanjani na ameanza mazoezi mepesi mepesi.

Samatta taarifa hizo amezitoa kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kuandika hivi “Nina furaha, kuanza mazoezi ya uwanjani baada ya kuwa nje kwa takribani miezi miwili kutokana na maumivu ya goti.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *