Mtoto wa Gaddafi kugombea urais wa Libya

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi, anatarajia kugombea urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2018.

Taarifa za Saif al-Islam kutaka kugombea nafasi hiyo ambayo baba yake alikuwa ameishikilia kwa muda wa miaka 42, ilitolewa na msemaji wa familia Basem Hashimi Soul.

“Saif al-Islam atagombea urais kwenye uchaguzi ujao ambao unaweza ukafanyika katikati mmwa mwaka 2018,ana dhamira ya kuongeza ulinzi zaidi na utulivu kulingana na jografia ya Libya, kwa kushirikiana na makundi yote ya Libya, hivi karibuni anatarajia kuweka wazi tarahe ya kujitangaza rasmi kwenye vyombo vya habari”, amesema msemaji Basem Hashimi Soul.

Nchi ya Libya hivi karibuni imekuwa isiyo ya utulivu, kutokana na vurugu zinazoendelea, huku mtoto huyo wa Gaddafi akiwa na imani kubwa Umoja wa Mataifa utakubaliana nae katika kipindi hiki kigumu ambacho nchi hiyo kinaipitia, cha kutafuta utulivu.

Saif al-Islam ni mtoto wa pili wa Muammar Gaddafi ambaye alitolewa madarakani na kuuawa mwaka 2011, na pia ni mwanasiasa mwenye utaalam wa uchumi.Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *