Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 26 Novemba.

Miaka 8 iliyopita katika siku kama ya leo, watu 200 waliuawa na wengine 300 kujeruhiwa katika mji wa Mumbai nchini India kufuatia mashambulio kadhaa ya kigaidi na mapigano ya siku tatu baina ya vikosi vya usalama na magaidi. Hoteli kubwa mbili na kituo kikuu cha treni katika mji huo wa kibiashara wa Mumbai ni miongoni mwa maeneo yaliyolengwa katika mashambulio hayo ya kigaidi. Serikali ya India iliibebesha lawama Pakistan na kuituhumu kwamba, ilihusika katika mashambulio hayo kwa madai kuwa, magaidi waliofanya mashambulizi hayo walipata mafunzo nchini Pakistan. Hata hivyo Pakistan ilikanusha madai hayo na kutangaza kuwa iko tayari kushiriki katika uchunguzi wa pamoja na India ili kuwasaka wahusika wakuu wa mashambulio hayo ya kigaidi.

Tarehe kama ya leo miaka miaka 161 iliyopita, Adam Bernard Mickiewicz mshairi na mwandishi mkubwa wa Kipoland aliaga dunia huko Istanbul uliokuwa mji mkuu wa utawala wa Othmania. Alizaliwa mwaka 1798. Kama alivyokuwa baba yake, Mickiewicz naye alikuwa mtu aliyekuwa akipigania uhuru. Aliishi katika zama ambazo nchi yake ya Poland ilikuwa imegawanywa na madola ya Prussia, Russia na Austria na alikuwa akifanya jitihada ili nchi yake iungane tena na kuwa kitu kimoja. Ni kutokana na sababu hiyo ndiyo maana mwaka 1823 alibaidishiwa nchini Russia. Baada ya miaka 6, Adam Mickiewicz alikimbilia nchini Ufaransa na kuanza kufundisha fasihi ya lugha.Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *