Hemedy PhD adai watoto wake 6 wamepishana miezi miwili, miwili tu

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Hemedy PhD amefunguka mambo kadhaa kuhusu yeye kuwa baba wa watoto sita.

Muimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma ‘January to December’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio katika watoto wake sita alionao wamepishana kila mmoja miezi miwili katika kuzaliwa.

“Mtoto wangu mkubwa ana miaka mitatu waliofuatia wote wanapishana miezi miwili miwili, sitaki drama kila mtu na mama yake lakini all in all nawapenda sana watoto wangu na itakuja siku nitaweka mambo yote wazi kama mnyama future” amesema.

Katika hatua nyingine Hemedy amesema wiki mbili zilizopita girlfriend wake alipata shida na alikuwa amebeba mapacha, hivyo sasa angekuwa na watoto nane akiwa na umri wa miaka 29.Share:

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *