Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 21 Novemba.

Na miaka 234 iliyopita sawa na tarehe 21 Novemba mwaka 1783, kwa mara ya kwanza katika historia ya jitihada za mwanadamu za kupaa angani, puto lilitumwa angani. Puto hilo lilikuwa limepandwa na watu wawili mmoja akiwa mwanafizikia wa Ufaransa aliyejulikana kwa jina la Pilatre De Rozier. Tangu alipokuwa masomoni De Rozier alikuwa akifikiria kutengeneza nyenzo ya kupaa angani na kwa kutengeneza puto hilo mwanafizikia huyo akawa amefanikiwa kuruka angani.

Siku kama ya leo miaka 26 iliyopita, Butros Butros Ghali alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa sita wa Umoja wa Mataifa. Butros Ghali alizaliwa mwaka 1922 katika mji mkuu wa Misri Cairo. Baada ya kumaliza masomo yake Butros Butros Ghali alianza kufundisha katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Siasa cha Cairo. Mwanadiplomasia huyo ndiye aliyemshawishi Anwar Sadat Rais wa zamani wa Misri kutia saini mkataba wa Camp David mwaka 1978 na katika kuutambua rasmi utawala wa Israel.

Katika siku kama ya leo miaka 21 iliyopita, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliitangaza na kuiainisha siku hii ya tarehe 21 Novemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Televisheni. Lengo la Umoja wa Mataifa la kuianisha siku hii lilikuwa ni kuweko mabadilishano ya vipindi vya runinga hususan vipindi vinavyotayarishwa kwa lengo la kueneza amani, ustawi wa kijamii, kiuchumi na kuimarisha masuala ya kiutamaduni ya jamii.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *