Leo katika historia : Siku kama ya leo miaka 71 iliyopita mvua bandia ya kwanza ilitengenezwa

Siku kama ya leo miaka 71 iliyopita, yaani tarehe 16 Novemba mwaka 1946, kwa mara ya kwanza ilitengenezwa mvua bandia. Mvumbuzi wa mvua hiyo aliyekuwa mtaalamu wa masuala ya hali ya hewa wa Marekani akishirikiana na mwanakemia mmoja wa nchi hiyo, walitumia gesi ya kaboni na hewa katika kutengeneza mvua hiyo. Mvua bandia hutumiwa katika maeneo yenye ukame au yenye uhaba wa mvua.

Na siku kama ya leo miaka 72 iliyopita sawa na tarehe 16 Novemba mwaka 1945, vikosi vya jeshi la Ufaransa viliishambulia Vietnam na kuanza mapambano ya muda mrefu ya wananchi kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo. Baada ya karne moja ya kukoloniwa Vietnam na Ufaransa, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia Japan iliidhibiti nchi hiyo. Japan iliondoka Vietnam baada ya kushindwa katika vita hivyo, na Vietnam ikaanza kukaliwa kwa mabavu na Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

×

Like us on Facebook