Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 4 Novemba.

Katika siku kama ya leo miaka 61 iliyopita, kufuatia kuongezeka upinzani dhidi ya utawala wa kikomonisti huko Hungary, Jeshi Jekundu la Umoja wa Kisovieti liliikalia kwa mabavu nchi hiyo. Baada ya kifo cha Joseph Stalin, kiongozi dikteta wa Umoja wa Kisovieti 1953 na kupatikana anga ya wazi kwa kiwango fulani kupitia kwa mrithi wake Nikita Khrushchev, baadhi ya nchi za Kikoministi za Ulaya zilitaka kuweko anga ya wazi zaidi. Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Magharibi vilikuwa vikiwahamasisha wananchi na kuwataka waanzishe harakati na mapambano. Hapo ndio wananchi wa Hungary walipoanzisha harakati dhidi ya utawala wa nchi yao na kuwauwa Wakoministi kadhaa.

Na katika siku kama ya leo miaka 22 Waziri Mkuu wa wakati huo wa  Israel Yitzhak Rabin aliuawa kwa kupigwa risasi na Muisrael mwenzake mwenye misimamo mikali. Rabin alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa utawala wa Israel kwa tiketi ya chama cha Leba katika mwaka 1974 na kuongoza hadi 1977. ambapo alilazimika kujiuzulu kutokana na ubadhirifu wa mali ya umma. Alichaguliwa tena kuwa Waziri Mkuu wa Israel mwaka 1992. Mauaji ya Yitzhak Rabin yaliyofanywa na Myahudi mwenzake Yigal Amir .

Miaka 99 iliyopita katika siku kama ya leo, Ufalme wa Austria-Hungary ulisalimu amri kwa waitifaki ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kufikia tamati Vita vya Kwanza vya Dunia. Utawala huo ambao ndio uliokuwa umeanzisha vita, ulikuwa ukihesabiwa kuwa muitifaki muhimu wa Ujerumani. Hata hivyo kutokana na kushindwa mara nyingi katika vita, ulikubaliana na masharti ya kuacha vita. Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, utawala wa Austria-Hungary uligawanywa kwa nchi kadhaa na ukoo wa Habsburg uliokuwa ukitawala ukasambaratika.

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *