Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 29 octoba

Siku kama ya leo miaka 84 iliyopita alifariki dunia Léon Charles Albert Calmette mgunduzi wa chanjo ya BCG. Albert Calmette alikuwa tabibu mtajika na mahiri wa Kifaransa ambaye alihitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Paris. Chanjo ya B.C.G hutumika kukinga maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu au TB. Kugunduliwa chanjo hiyo kumepunguza vifo vya watu wanaopatwa na ugonjwa wa TB duniani kote.

Siku kama ya leo vilevile mwaka 1959 alizaliwa Rais wa awamu ya 5 wa Tanzania Mh John Pombe Joseph Magufuli.

Na katika siku kama ya leo miaka 94 iliyopita, mfumo wa utawala wa serikali ya jamhuri uliasisiwa nchini Uturuki kwa uongozi wa Rais Mustafa Kemal mashuhuri kwa jina la Ataturk. Kemal Ataturk aliiongoza kidikteta nchi hiyo kwa muda wa miaka 15.

Siku kama ya leo miaka 234 iliyopita alifariki dunia Jean le Rond d’Alembert, mtaalamu wa hisabati wa Ufaransa. Rond d’Alembert alizaliwa mjini Paris tarehe 15 Novemba mwaka 1717. Pamoja na hayo baba na mama yake walimtelekeza kando na kanisa moja la mjini Paris. Kuanzia wakati huo alilelewa na mwanamke mmoja mchuuzi wa mji huo na kuanza kumpatia mafunzo mbalimbali kama mtoto wake. Akiwa na miaka 22 aliandika makala kuhusiana na masuala ya hesabu na baada ya hapo akaanza kupata umashuhuri. Miaka kadhaa baadaye aliendeleza kazi zake za kielimu na kuwasilisha mbinu mpya ya kimahesabu ambayo ilikuwa na jibu kwa kila muamala wa Aljebra. Hata kama Jean le Rond d’Alembert alifanya juhudi kubwa kuvumbua mbinu hiyo, lakini ilikuja kuthibitishwa kwa mara ya kwanza miaka 16 baadaye akiwa amekwishafariki dunia. Msomi huyo alifariki dunia Oktoba 29 1783  akiwa na umri wa miaka 66.Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *