Ushindi wa Bondia Anthony Joshua dhidi ya Takam wazua gumzo uwanjani.

Jana usiku kulikuwa na pambano kubwa la masumbwi kati ya Bondia Muingereza, Antony Joshua na bondia Carlos Takam kutoka Cameroon. Ambapo Joshua alimaliza pambano kwa kumtwanga Takam kwa TKO iliyoleta utata kwa mashabiki.

Joshua alipata ushindi wa TKO kunako raundi ya 10 kwa refa kusimamisha pambano hilo baada ya Takam kuvuja damu nyingi usoni.

Watu wengi waliohudhuria kwenye pambano hilo walimzomea mwamuzi wa pambano hilo wakidai Takam alikuwa bado ana nguvu ya kupambana japokuwa alikuwa amepasuka usoni.

Mashabiki wengi wa Takam wanasema refa angempa muda bondia huyo kufutwa damu ili aendelee na pambano kwani alikuwa bado na nguvu za kurusha ngumi hivyo wanaamini mwamuzi huyo alimaliza pambano kwa matakwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mpambano huo, Anthony Joshua amesema kama pambano lingeendelea angemuumiza zaidi Takam hivyo maamuzi ya refa yalimuokoa .

Huu unakuwa ni ushindi wa 20 mfululizo kwa Antony Joshua (28) baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa mkanda wa IBF hapo jana.

Tokeo la picha la anthony joshua carlos takam

Tokeo la picha la anthony joshua carlos takam

Tokeo la picha la anthony joshua carlos takamAuthor: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *