leo katika historia duniani : Siku kama ya leo miaka 236 iliyopita Marekani ilijipatia uhuru wake.

Miaka 236 iliyopita katika siku inayofanana na ya leo,Charles Cornwallis,kamanda wa kikosi cha wanajeshi wa Uingereza nchini Marekani alisalimu amri mbele ya George Washington, kamanda wa kikosi cha wanajeshi wa Marekani na kwa msingi huo vita vya kuikomboa Marekani vikamalizika rasmi.Vita hivyo vilianza mwaka 1775 kati ya wahajiri wa Kimarekani na wakoloni wa Kiingereza. Miaka miwili baada ya ushindi wa mwisho wa wahajiri, pande mbili hizo zilisaini makubaliano mwaka 1783 ambapo kwa mujibu wake Uingereza ilitambua rasmi uhuru wa Marekani.

Siku kama ya leo miaka 72 iliyopita, vita kati ya vikosi vya Japan na jeshi la Marekani vilianza katika visiwa vya Ufilipino. Itakumbukwa kuwa, wakati wa kuanza Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, Ufilipino ilishambuliwa na Japan na kwa muda mfupi ikawa imedhibitiwa na kukaliwa kwa mabavu. Hata hivyo baada ya kushindwa Ujerumani ya Kinazi katika Vita vya Pili vya Dunia, majeshi ya Marekani chini ya usimamizi wa Douglas MacArthur yaliishambulia Ufilipino na kuyatoa majeshi ya Japan katika ardhi ya nchi hiyo na kisha kuanzisha kambi za kijeshi nchini humo.Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *