Wema Sepetu: Umaarufu Unani ‘Cost’

MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Wema Sepetu, analia na umaarufu mkubwa alionao kwani umemfanya kushindwa kufanya vitu vingi ambavyo kama binadamu, na yeye alitamani kufanya.

Akiwa hajawahi kupanda daladala kwa miaka 11 sasa, tangu alipovikwa taji la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema al-isema akiwa ndani ya gari lake barabarani, hujisikia raha sana kuona watu wakiwa wamepanda usafiri huo, wakiwa wanazungumza na kucheka, kitu ambacho anakimiss sana, lakini hamna namna anayoweza kufanya.

“Unajua kiukweli kabisa natamani mno kupanda daladala, k w a sababu hata mimi ni binadamu, kuna kipindi natamani kupanda gari kutoka kwangu mpaka Kariakoo au mpaka Mbagala, lakini unafikiria utakapopanda itakuwa ni vurugu na siyo starehe tena, huu umaarufu kwa kweli unani-’cost’ sana wakati mwingine,” alisema Wema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

×

Like us on Facebook