CCTV kamera imeondolewa sehemu aliyopigwa risasi Mh. Lissu

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Mwenyekiti wake, Freeman Aikaeli Mbowe amesema kwa taarifa zao za kiuchunguzi zinasema kwamba CCTV kamera imeondolewa sehemu aliyopigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mbowe amesema kuwa eneo hilo ni jirani na waziri na kwenye nyumba ya waziri kuna CCTV kamera bila kumtaja waziri huyo ni nani.

“Katika makazi kuna kamera za kuchukua matukio yote yanayotokea katika makazi yetu ambayo yana vyombo vya ulinzi na usalama masaa 24 wenye silaha haiwezekani mtu akashabuliwa kwa kiwango kile mchana saa 7. Mhe. Lissu ni jirani wa Waziri kwenye nyumba ya Waziri kuna kamera ya CCTV kamera zetu za kiuchunguzi ni kwamba ile CCTV kamera imeondolewa, imeondolewa na nani, kwasababu gani na ilipelekwa wapi,? alihoji Mbowe.

Katika hatua nyingine Mbiwe alisema kuwa “limeanzia kwa Lissu na kuna wengine miongoni mwetu tuko kwenye wanted list, huu ni utamaduni ambao hatukuuzoea kwenye nchi yetu. Kwahiyo hatuwezi kulichukulia kama jambo jepesi.”

Mbunge Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu, eneo la ‘area D’ mjini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *