Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 08 octoba

Na miaka 12 iliyopita katika siku kama leo, mtetemeko mkubwa wa ardhi uliokuwa na ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha richta uliyakumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa Pakistan. Kitovu cha mtetemeko huo kilikuwa katika mji wa Muzaffarabad. Watu wapatao 90 elfu walipoteza maisha yao na wengine milioni 3 na laki 6 kubaki bila makazi kufuatia mtetemeko huo.

Siku kama ya leo miaka 77 iliyopita yaani 1940,Marekani iliwashauri raia wake kuondoka mashariki ya kati ingawa bado ilikuwa haijaanzisha vita na japan.Marekani na Japan walipigana vita mnamo terehe 8 disemba mwaka 1941.

Siku kama ya leo miaka 136 iliyopita, kimbunga kikali kiliikumba nchi ya Vietnam. Kimbunga hicho ambacho kililiathiri zaidi eneo la kusini mwa nchi hiyo, kiliharibu nyumba, miundombinu na mashamba. Kimbunga hicho kikubwa kilisababisha karibu watu laki tatu kufariki dunia.

Siku kama ya leo miaka 44 iliyopita yaani 1973 radio ya kwanza ya kibiashara LBC ilianza kurusha matangazo yake huko uingereza

Siku kama ya leo miaka 106 iliyopita, vilianza vita vya Balkan kwa ushiriki wa Bulgaria, Serbia na Ugiriki dhidi ya dola la Othmania. Mtawala wa Othmania kwa kipindi cha miaka kadhaa alikuwa akipanua utawala wake katika maeneo ya magharibi mwa Asia, kaskazini mwa Afrika na mashariki mwa Ulaya. Katika kipindi hicho wimbi la kutaka kujitawala katika nchi zilizokuwa chini ya utawala huo wa Othmani, lilisababisha kuibuka vita vingi ambapo vita vya Balkan vilikuwa mojawapo. Sababu ya kuibuka vita hivyo vya Balkan ambavyo vilianza Oktoba 1911 ilitokana na hatua ya utawala wa Othmania kukataa kuzipatia uhuru nchi zilizokuwa chini yake kama vile, Serbia, Bulgaria, Ugiriki na Montenegro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

×

Like us on Facebook