Utajiri wa Nay wapukutika.

VYUMA vimekaza! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya utajiri wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kudaiwa kwisha baada ya magari ya thamani aliyokuwa akiyamiliki kupukutika.

Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu ambaye ni mmoja wa watu wa karibu wa Nay, kwa sasa mwanamuziki huyo ana hali ngumu kimaisha kwani ule utajiri aliokuwa nao awali, kwa sasa haupo tena, umepukutika.

“Kiukweli mambo ni magumu sana kwa Nay kwa sababu magari yote aliyokuwa nayo ameuza na sasa amebaki na moja tu, ndiyo maana hata huoni akiwa na mbwembwe kama zamani, hapana chezea hali ngumu ya sasa wewe,” kilisema chanzo hicho.

Mnyetishaji huyo alizidi kutiririka kuwa, hata kwenye studio yake iliyopo Sinza-Kijiweni, Dar, kwa sasa wapo wakurugenzi wawili na kila mmoja ana timu yake ambapo mmojawapo ni Nay na mwingine alitajwa kwa jina moja la Isihaka.

“Studio kwake kwenyewe siku hizi hata hapaeleweki maana kuna uongozi wa watu wawili na kila mmoja ana watu wake. Kuna kipindi wanashindwa kuelewana katika mambo f’lani ya kiutendaji na vikao vimekuwa vikiwekwa kila kukicha,” alisema mtoa habari wetu.

Ili kuujua ukweli  alitafutwa mhusika mkuu Nay ambapo alikana tuhuma hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

×

Like us on Facebook