Gigy Money aumbuliwa kudanganya thamani halisi ya mavazi.

Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameumbuka baada ya kufanya mahojiano na runinga moja akisema kuwa, mavazi aliyovaa yalimgharimu shilingi milioni moja na laki tano kisha wajuzi wa mambo wakamuumbua.

Akizungumza juu ya ishu hiyo ambayo ilizua mjadala mzito, mmoja wa vyanzo makini alisema kuwa, hata viatu alivyovaa alidai kuwa vya shilingi laki mbili lakini ukweli ni kwamba vinauzwa shilingi elfu thelathini.

Kwa upande wake Gigy alisema kuwa, anawashangaa wanaojadili suala hilo kwa sababu yeye ndiye anayejua ukweli.

“Mimi ndiye mnunuzi, watu wanapaswa kukumbuka tu kila kitu kina bei tofauti kutokana na muuzaji na sehemu kinapouzwa,” alisema Gigy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

×

Like us on Facebook