Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 23 august

Siku kama ya leo miaka 73 iliyopia mji wa Paris ulikombolewa kutoka kwenye uvamizi wa Ujerumani. Miezi 15 baada ya kushtadi moto wa Vita vya Pili vya Dunia dikteta Adolph Hitler aliyaamuru majeshi ya nchi hiyo kuushambulia mji wa Paris kwa lengo la kutaka kuudhibiti. Tarehe tano Juni mwaka 1940, Hitler alitoa amri ya kuharibiwa kikamilifu muundo wa majeshi ya Ufaransa ambapo siku tatu baadaye yaani tarehe nane Juni mwaka 1940, vikosi vya majeshi ya Wanazi vilikishinda kikosi cha ulinzi cha Ufaransa katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na jeshi la Ujerumani likaingia nchini Ufaransa bila ya upinzani wowote. Mji wa Paris ulikaliwa kwa mabavu na Ujerumani kwa kipindi cha miaka 4 na ulikombolewa katika siku kama hii ya leo baada ya Wajerumani kushindwa mtawalia katika medani mbalimbali za vita. Mji huo ulikombolewa na majeshi ya waitifaki.

Siku kama ya leo ya tarehe 23 ya mwezi wa 8.Aliyekuwa kiongozi mkuu wa Alqaida Osama Bin Laden atuma barua rasmi iliyotangaza vita dhidi ya taifa la marekani.

Vilevile siku kama ya leo alizaliwa mchezaji nguli wa kikapu duniani Kobe Bryant

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

×

Like us on Facebook