Volkswagen zapigwa marufuku Uswizi

Taifa la Uswizi limepiga marufuku kuuzwa kwa magari aina ya Volkswagen ambayo yana mitambo  iliyotengenezwa kudanganya majaribio ya gesi chafu.Idara inayosimamia usafiri wa barabarani nchini humo inasema kuwa hadi magari 180,000 yataathiriwa.

Hilo ndilo pigo la hivi punde kwa kampuni hiyo ya Ujerumani tangu ikiri kuwa magari milioni 11 yanayotumia mafuta ya diesel kote duniani yamewekwa mitambo inayuweza kudanganya kuhusu gesi chafu.Mauzo ya hisa za kampuni ya Volkswagen yameshuka katika kipindi cha wiki moja tangu kufichuliwa kwa sakata hiyo.Mkurugenzi mpya wa kampuni ya Volkswagen amesema kuwa uchunguzi ulio wa kina na wazi utafanyika.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na admin
muda 2015-09-26 05:37:57
Watazamaji 678
Volkswagen zapigwa marufuku Uswizi
Uko hapa : Home > teknolojia>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo