Lewandowski avunja rekodi ya mabao

Robert Lewandowski alifunga mabao matano katika dakika tisa baada ya kuingia uwanjani kama nguvumpya wa Bayern Munich mechi ya Bundesliga dhidi ya Vfl Wolfsburg.Bayern walikuwa nyuma 1-0 wakati wa mapumziko, wakati Lewandowski alipoingia kuchukua nafasi ya for Thiago.Dakika sita baadaye, mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland alifunga bao lake la kwanza mechi hiyo kutoka karibu na goli.Huo ulikuwa tu mwanzo wa ngoma. Lewandowski aliongeza mengine manne upesi na kuweka rekodi ya mabao matano ya kasi Zaidi kufungwa na mchezaji mmoja katika historia ya ligi kuu ya soka ya Ujerumani Bundesliga.Wolfsburg, waliomaliza nambari mbili ligini nyuma ya Bayern msimu uliopita, walikuwa wametwaa uongozi kupitia bao la Daniel Caligiuri.Wageni hao nusura waongeze jingine kupitia kombora la hatua 60 kutoka kwenye goli lililotumwa na Josuha Guilavogui, lakini kombora hilo lilitoka nje.Lakini kuingizwa uwanjani kwa Lewandowski, 27, kulibadilisha mambo na kufuta matumaini yao kabisa.

Ushindi huo uliwezesha vijana hao wa Pep Guardiola kufika kileleni kwenye jedwali, alama tatu mbele ya Borussia Dortmund, watakaokutana na Hoffenheim Jumatano. Wolfsburg wanashikilia nafasi ya tatu.

Lewandowski alifunga mabao mengi ligini kwa dakika tisa kushinda ...

  • Mabao ambayo Liverpool, Newcastle na West Brom wamefunga msimu huu
  • Mabao ambayo klabu sita za mwisho Bundesliga zimefunga
  • Mabao ambayo Wayne Rooney amefunga 2015
  • Mabao Mario Balotelli alifunga alipokuwa Liverpool
  • Mabao ambayo Nicklas Bendtner amefunga katika kipindi cha miaka mitatu
imewekwa na admin
muda 2015-09-23 16:39:37
Watazamaji 899
Lewandowski avunja rekodi ya mabao
Uko hapa : Home > michezo>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo