Leo hii katika historia tarehe 24 mwezi wa tisa.
imewekwa na admin
muda 2016-09-24 07:19:23
Watazamaji 558
Leo hii katika historia tarehe 24 mwezi wa tisa.
Uko hapa : Home > je wajua / kumbukumbu muhimu>

Leo tarehe 10 Dhilhaj ni moja ya sikukuu kubwa za Kiislamu. Katika siku hii mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu waliokwenda Makka, huchinja mnyama kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mola wao na kuhuisha kumbukumbu ya Nabii Mtukufu Ibrahim.Mwenyezi Mungu aliijaribu imani  ya Nabii huyo kwa kumwamuru amchinje mwanawe kipenzi Ismail.Licha ya mashaka ya utekelezwaji wa amri hiyo, Nabii Ibrahimu aliandaa mazingira ya kutekeleza amri hiyo na kumlaza chini mwanaye na kuanza kuikata shingo yake lakini kisu kilikataa kuchinja. Hapo ndipo alipoambiwa na Mwenyezi Mungu kuwa amefaulu mtihani huo na akamtumia mnyama wa kuchinja badala ya mwanaye Ismail. Tukio hili lenye yakinifu na mafunzo tele linawapa wanadamu somo la kujitoa mhanga, kujisabilia kwa ajili ya mwenyezi mungu, kushinda matamanio na matakwa ya nafsi na kusalimu amri mbele ya amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu.Tabelltz.com inatoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu kote duniani kwa mnasaba wa sikukuu hii kubwa.

Katika siku kama ya leo miaka 105 iliyopita alizaliwa Konstantin Chernenko kiongozi wa mwisho wa Umoja wa Kisovieti kabla ya Mikhail Gorbachev. Akiwa na umri wa miaka 18 alikuwa kiongozi katika Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Kikomonisti. Baada ya Konstantin Chernenko kufariki dunia, Mikhail Gorbachev alimrithi kiti cha uongozi wa Umoja wa Kisovieti.

Siku kama ya leo miaka 77 iliyopita, ndege za Ujerumani zilianza kufanya mashambulio ya mabomu katika mji mkuu wa Poland Warsaw. Mashambulio hayo ya mabomu yalidumu kwa muda wa siku tatu wakati wa kuanza Vita Vikuu vya Pili vya Duni. Adolph Hitler, Kiongozi wa Ujerumani ya Kinazi alikuwa ametoa amri ya kudhibitiwa mji huo kwa gharama yoyote ile

Na siku kama ya leo miaka 41 iliyopita, Guinea Bissau ilitangaza uhuru wake kutoka kwa mkoloni Mreno. Guinea Bissau iligunduliwa mwaka 1446 na Mwana Mfalme Henry aliyekuwa akitawala Ureno pamoja na wenzake na kuwa koloni la nchi hiyo. Guinea Bissau ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Guinea Ureno, ilikuwa miongoni mwa vituo vya biashara ya utumwa ya wazungu katika karne za 17 na 18. Na hatimaye ilipofika mwaka 1974, Ureno ikakubali kuwa huru nchi ya Guinea Bissau. Guinea Bissau iko kaskazini magharibi mwa Afrika na katika pwani ya bahari ya Atlantic.

 

Unasemaje kuhusu hii?

Hamisi mohamedi alisema, tarehe 2015-08-10 18:07:58:
Nataka download nyimbo zote

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
HABARI ZA KIMATAIFA
Bookmark and Share
deSiGned by sundo