Leo katika historia jumanne ya tarehe 22/09/2015
imewekwa na admin
muda 2015-09-22 04:39:10
Watazamaji 548
Leo katika historia jumanne ya tarehe 22/09/2015
Uko hapa : Home > je wajua / kumbukumbu muhimu>

Na siku kama ya leo miaka 35 iliyopita, majeshi ya dikteta wa zamani wa Iraq Saddam Hussein yalianza mashambulio makubwa ya anga na nchi kavu dhidi ya  Iran na hivyo kuanzisha vita vya miaka minane dhidi ya Iran. Jeshi la Iraq lilikuwa limefanya uvamizi na mashambulizi kadhaa katika maeneo ya mpakani ya Iran miezi kadhaa nyuma. Magari ya deraya na vikosi 12 vya jeshi la nchi kavu la Iraq viliyashambulia maeneo ya mipaka ya kusini magharibi mwa Iran. Mapambano makali ya wananchi wa Iran yaliwalazimisha askari wa Saddam kurejea nyuma hadi kwenye mipaka inayotambulika kimataifa.

Siku kama ya leo miaka 56 iliyopita, nchi ya Mali iliyo kaskazini magharibi mwa Afrika ilijipatia uhuru. Karibu miaka elfu mbili iliyopita nchi ya Mali ilikuwa na utamaduni mkubwa. Hata hivyo nchi hiyo tangu karne ya 18 hadi ya 19 Miladia ilikuwa moja ya tawala za ufalme wa Sudan. Baada ya Morocco kutwaa baadhi ya maeneo yaliyokuwa chini ya tawala za ufalme wa Sudan ikiwemo Mali, tawala mbalimbali za kikabila nchini Mali zilifanikiwa kuingia madarakani. Satwa ya Wafaransa nchini Mali ilianza mnamo karne ya 19 na hadi kufikia mwaka 1898 nchi hiyo ilikuwa chini ya usimamizi wa Ufaransa. Hata hivyo Mali ambayo ilikuwa ikiitwa Sudan ya Ufaransa, mwaka 1958 ilianza kujitawala na mwaka 1960 ikajipatia uhuru wake kamili.

Unasemaje kuhusu hii?

mussa alisema, tarehe 2015-08-01 08:43:02:
naipenda tabelltz

Deogracias lucas alisema, tarehe 2015-08-12 05:46:56:
ebhna b!g up xana {tabell} na iyo ngoma jamaa yuko poa xana i mean maitendea hak iy video..

RAPHAEL alisema, tarehe 2015-09-01 02:49:03:
FOR NOW TANZANIA GOING UP ON MUSIC ,KEEP IT ON FOR ALL PEOPLE THEY LIKE OUR TALENT ,FOR I CAN SAY NICE SONG AND VIDEO LOVEEEEE ALLL

denis alisema, tarehe 2016-05-08 14:15:24:
amejitahd kaka akaze

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
HABARI ZA KIMATAIFA
Bookmark and Share
deSiGned by sundo