Je waju?..Madhara ya Kiafya Kuhusu Wanaojichora Tattoo.
imewekwa na Kibonde
muda 2017-01-06 02:40:28
Watazamaji 309
Je waju?..Madhara ya Kiafya Kuhusu Wanaojichora Tattoo.
Uko hapa : Home > je wajua / kumbukumbu muhimu>

Tafiti nyingi za kitabibu pia zinaonesha kwamba, wino au rangi za tattoo zinaweza kusababisha uambukizo wa bakteria aina ya Mycobacterium cholonae.

Bakteria hawa wanaweza kusababisha magonjwa ya ngozi na nyama za mwili, matatizo ya njia ya mkojo, mfumo wa kupumua, magonjwa ya uambukizo kwenye mifupa na nyama za moyo.

Michoro hiyo pia huweza kusababisha homa ya uti wa mgongo na tatizo la macho.
Vilevile, vifaa vinavyotumiwa kuchora mapambo hayo hutumika kwa watu mbalimbali kwa wakati mmoja bila utaalamu sahihi wa kuvisafisha.
Hali hiyo huweza kusababisha vibebe vimelea vya magonjwa mbalimbali na kuyahamishia kwa wengine.

Hali hii inaweza kusababisha uambukizo wa magonjwa yatokanayo na virusi hatari kama vile virusi vya Ukimwi, virusi ninavyosababisha homa ya ini (Hepatitis B na C) au virusi vya malengelenge (herpes simplex virus).

Kumbuka, wakati wa kuchora tattoo, ngozi hutobolewa kwa mashine au sindano hadi kuifikia sehemu ya ndani kabisa. Hii ni hatari kwa afya yako.

Unasemaje kuhusu hii?

Baba Chriss alisema, tarehe 2014-08-29 18:55:30:
Kiukweli samir amejituma vya kutosha kwenye huu wimbo Mungu akutangulie na kukusaidia kwa kila jambo.

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
HABARI ZA KIMATAIFA
Bookmark and Share
deSiGned by sundo