Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 04 Desemba
imewekwa na admin
muda 2016-12-04 00:36:38
Watazamaji 630
Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 04 Desemba
Uko hapa : Home > je wajua / kumbukumbu muhimu>

Miaka 117 iliyopita, kwa mara ya kwanza chanjo ya homa ya matumbo au Typhoid ilitumiwa kwa mwanadamu ili kukabiliana na maradhi hayo ambayo husababisha kuhara damu. Awali chanjo hiyo ilivumbuliwa na mtafiti mmoja wa Kifaransa na baadaye ilikamilishwa na tabibu wa Kiingereza kwa jina la Almroth Edward Wright.

Na Miaka 64 iliyopita, yaani mwaka 1952 katika siku kama ya leo, mkutano wa pande tatu wa Marekani, Uingereza na Ufaransa ulifanyika katika kisiwa cha Bermuda kaskazini mwa Amerika Kusini. Mbali na nchi hizo tatu kujadili uhusiano baina yao, zilichukua maamuzi muhimu na kuratibu namna ya kukabiliana na siasa za Shirikisho la Umoja wa Sovieti huko Berlin. Katika zama hizo sehemu ya magharibi ya mji wa Berlin, Ujerumani ilikuwa chini ya udhibiti wa Marekani, Uingereza na Ufaransa na sehemu ya mashariki ilikuwa chini ya udhibiti wa Umoja wa Sovieti. Kupamba moto hitilafu za namna ya kuuendesha mji huo, ndiko kulikopelekea kujengwa ukuta maarufu wa Berlin mnamo mwaka 1961.

Katika siku kama ya leo miaka 337  iliyopita yaani mwaka 1679 Thomas Hobbes mwanafalsafa mashuhuri wa Kiingereza aliaga dunia. Alizaliwa tarehe tano Aprili mwaka 1588 Miladia. Alimaliza masomo yake katika Chuo Kikuu Oxford nchini Uingereza na alifanya utafiti mkubwa kuhusiana na falsafa. 

Aliathiriwa sana na fikra za mwanafalsafa Mtaliano Niccolò Machiavelli na alijifunza mengi kutokana na yaliyokuwa yakijiri duniani. Aliamini kuwa mfalme alipaswa kuwa na utawala usio na mipaka na kwamba watu hawapaswi kulalamikia mtawala hata kama malalamiko yao ni sahihi na kwamba walalamikaji walipaswa kukandamizwa. Mwanafalsafa huyo wa Kiingereza alifariki dunia  tarehe 4 Desemba mwaka 1679 akiwa na umri wa miaka 91.

 

Unasemaje kuhusu hii?

farhad Mohammed alisema, tarehe 2014-09-04 12:17:23:
wazzea Muko juu tu sana big up Jo

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
HABARI ZA KIMATAIFA
Bookmark and Share
deSiGned by sundo