Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 29 octoba
imewekwa na admin
muda 2016-10-29 02:01:09
Watazamaji 756
Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 29 octoba
Uko hapa : Home > je wajua / kumbukumbu muhimu>

Siku kama ya leo miaka 83 iliyopita alifariki dunia Léon Charles Albert Calmette mgunduzi wa chanjo ya BCG. Albert Calmette alikuwa tabibu mtajika na mahiri wa Kifaransa ambaye alihitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Paris. Chanjo ya B.C.G hutumika kukinga maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu au TB. Kugunduliwa chanjo hiyo kumepunguza vifo vya watu wanaopatwa na ugonjwa wa TB duniani kote.

Na katika siku kama ya leo miaka 93 iliyopita, mfumo wa utawala wa serikali ya jamhuri uliasisiwa nchini Uturuki kwa uongozi wa Rais Mustafa Kemal mashuhuri kwa jina la Ataturk. Kemal Ataturk aliiongoza kidikteta nchi hiyo kwa muda wa miaka 15 na kufanya hujuma za kufuta sheria, nembo pamoja na matukufu ya Kiislamu na wakati huo huo, kueneza utamaduni na nembo za Kimagharibi nchini humo. Hata baada ya kufariki dunia kiongozi huyo aliyekuwa na uadui na Uislamu mnamo mwaka 1938, njama hizo dhidi ya Uislamu nchini Uturuki ziliendelezwa na wafuasi wake.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
HABARI ZA KIMATAIFA
Bookmark and Share
deSiGned by sundo