Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 25 octoba
imewekwa na admin
muda 2016-10-25 08:32:34
Watazamaji 543
Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 25 octoba
Uko hapa : Home > je wajua / kumbukumbu muhimu>

Siku kama ya leo, miaka 205 iliyopita, alizaliwa Évariste Galois, mtaalamu wa hesabati wa Ufaransa, karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Paris. Hadi umri wa miaka 12, Galois hakuwahi kufundishwa na mtu yeyote isipokuwa mama yake na alijiunga na chuo akiwa na umri huo na kuanza kusoma vitabu mbalimbali vya taaluma ya hisabati. Aliandika kitabu chake cha kwanza mashuhuri cha hisabati akiwa na umri wa miaka 18 na baada ya hapo aliandika vitabu vitatu vipya katika taaluma hiyo na kujipatia umashuhuri mkubwa. Galois alifungwa jela kutokana na itikadi zake za kisiasa na aliuawa akiwa na umri wa miaka 21 hapo tarehe 29 mwezi Mei mwaka 1832. 

Siku kama ya leo miaka 135 iliyopita, alizaliwa Pablo Picasso mchoraji mashuhuri wa Kihispania. Picasso alikuwa mwasisi wa harakati ya Cubist ambayo ilienea kwa kasi kubwa miongoni mwa wachoraji wa Ufaransa. Pablo Picasso alichora picha nyingi na daima alikuwa akifanya juhudi za kuendeleza harakati hiyo. Mchoro wa 'The Girls of Avignon' wa mchoraji huyo ndio uliokuwa mwanzo wa mtindo wa Cubism na kazi kubwa zaidi ya Picasso katika mtindo huo ni 'Guernica'. Katika mchoro huo Pablo Picasso anaonesha hofu iliyompata kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za Ujerumani na Italia dhidi ya mji wa Guernica. Picasso alifariki dunia Aprili mwaka 1973.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
HABARI ZA KIMATAIFA
Bookmark and Share
deSiGned by sundo