Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 21 octoba
imewekwa na admin
muda 2016-10-21 04:05:28
Watazamaji 539
Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 21 octoba
Uko hapa : Home > je wajua / kumbukumbu muhimu>

Miaka 183 iliyopita katika siku kama hii ya leo, alizaliwa Alfred Nobel mkemia wa Sweden na mvumbuzi wa dynamite. Nobel alikuwa na shauku kubwa ya kujifunza sayansi ya kemia na baadaye akafanya utafiti mkubwa katika uwanja huo na kufanikiwa kuvumbua mada za mlipuko yaani (dynamite). Kinyume na alivyotarajia, majeshi ya nchi mbalimbali yalianza kutumia dynamite vitani na hivyo kusababisha mauaji ya raia wengi. Mkemia Nobel ambaye alikuwa na utajiri mkubwa na hakufikiri kuwa dynamite ingeweza kutumiwa vibaya, aliamua kutoa utajiri wake kama tuzo na zawadi. Alfred Nobel alifanya hivyo kwa lengo kwamba, tuzo hiyo itolewe kila mwaka kwa minajiri ya aliyefanya kazi kubwa ya thamani duniani katika masuala ya sayansi, fasihi na amani duniani.

Siku kama ya leo miaka 30 iliyopita Brigedia Jenerali Mundhir Abu Ghazala, kamanda Jeshi la Majini la Palestina aliuawa na maajenti wa shirika la ujasusi la utawala wa Israel Mossad.Walimuuwa kigaidi kamanda huyo wa jeshi la majini la Palestina kwa kutega bomu ndani ya gari lake huko Athens mji mkuu wa Ugiriki.

Siku kama ya leo miaka 226 iliyopita, alizaliwa malenga wa Kifaransa Alphonse de Lamartine.  De Lamartine alitambulika kuwa msanii na mwanafikra mkubwa nchini Ufaransa. Aliwahi pia kusafiri Mashariki na kuishi katika mji mkuu waBairut,Lebanon. Aidha miongoni mwa athari za malenga huyu, ni pamoja na "Safari ya Mashariki" na "Kimya cha Malaika".  Alphonse de Lamartine alifariki dunia mwaka 1869.

 

Unasemaje kuhusu hii?

bestemwamgema alisema, tarehe 2015-11-23 03:16:02:
nampongeza xn mh magufuli kwa kaz njul akiwa hivyo2 ata iko mboa nchi

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
HABARI ZA KIMATAIFA
Bookmark and Share
deSiGned by sundo