Leo hii katika historia tarehe 20 mwezi wa tisa.
imewekwa na admin
muda 2016-09-20 03:17:35
Watazamaji 1365
Leo hii katika historia tarehe 20 mwezi wa tisa.
Uko hapa : Home > je wajua / kumbukumbu muhimu>

Siku kama ya leo miaka 184 iliyopita, lilitengenezwa basi la kwanza lililokuwa likitumia nishati ya mvuke. Basi hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 30, huku likienda kwa mwendo mdogo na liligunduliwa na raia wa Uingereza kwa jina la Gordon Branz. Hii leo mabasi bora na ya kisasa yamegeuka kuwa moja ya vyombo muhimu vya usafiri.


Siku kama ya leo miaka 148 iliyopita, nchi ya Hungary iliungana na ardhi ya Austria na Francois Joseph akawa mtawala wa kifalme wa nchini mbili hizo. Hungary ambayo kwa mara kadhaa katika historia ilivamiwa na kukaliwa kwa mabavu na nchi zenye nguvu za Ulaya kama vile Austria na utawala wa Othmania, baadaye ilijipatia uhuru wake mnamo mwaka 1918 mwishoni mwa Vita vya Kwanza vya Dunia.


Siku kama ya leo miaka 36 iliyopita, Jean-Bedel Bokasa, dikteta wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi. Bokasa alizaliwa mnamo mwaka 1922 na kusomea nchini Ufaransa, huku akiwa shabiki mkubwa wa Napoleon Bonaparte na Charles de Gaulle, viongozi wawili wa zamani wa Ufaransa. Alichukua madaraka ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, mwaka 1966 baada ya kufanya mapinduzi dhidi ya binamu yake David Dacko, wakati Bokasa alipokuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo. Jean-Bedel Bokasa alitawala nchi hiyo kwa mfumo wa kiimla na kwa kipindi cha miaka 13 sanjari na kusimamia moja kwa moja wizara 14 kati ya wizara 16 za taifa hilo la katikati mwa Afrika.

HABARI ZA KIMATAIFA
Bookmark and Share
deSiGned by sundo