Jeshi la Burkina Faso lawasili mji mkuu
imewekwa na admin
muda 2015-09-22 04:01:24
Watazamaji 469
Jeshi la Burkina Faso lawasili mji mkuu

Jeshi la Burkina Faso limefika mji mkuu wa Ouagadougou likilenga kushurutisha walinzi wa rais waliopindua serikali kusalimu amri.

Mashauriano kati ya wakuu wa jeshi na walinzi hao wa rais yanaendelea, duru zimesema.

Kiongozi wa mapinduzi Jenerali Gilbert Diendere alisema kwamba yuko tayari kurejesha mamlaka kwa uongozi wa kiraia, lakini baada tu ya mpango wake wa kumaliza mzozo wa sasa kuungwa mkono na viongozi wa mataifa ya eneo hilo.

Walinzi wa rais ni watiifu kwa kiongozi aliyetimuliwa mamlakani mwaka jana Blaise Compaore.

Walimzuilia Kaimu Rais Michel Kafando Jumatano iliyopita, na kumtangaza Jenerali Diendere kuwa kiongozi mpya.

Tangu wakati huo, watu 10 wameuawa kwenye makabiliano kati ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi hayo na maafisa wa usalama. Watu zaidi ya 100 wamejeruhiwa.

Balozi wa Ufaransa nchini Burkina Faso, Gilles Thibault, aliandika kwenye Twitter kwamba Bw Kafando ameachiliwa huru na sasa yumo kwenye makao ya balozi huyo.

Jumatatu, wanajeshi wa Burkina Faso waliamuru walinzi hao wa rais kuweka silaha chini kabla yao kufunga safari kuelekea mji mkuu.

"Lazima sasa tuhakikishe viongozi wa mapinduzi wanasalimu amri bila kuwepo kwa ufyatulianaji wa risasi au umwagikaji wa damu,” Kanali Serge Alain Ouedraogo, afisa mmoja mkuu nchini humo alisema.

Akiongea kutoka mafichoni, Jenerali Diendere aliambia BBC: “Kuwa tayari kusalimu amri? Hatujafika huko bado …Tungependa kuendelea na mazungumzo na tunawaambia wote kwamba tuko tayari kutekeleza maamuzi ya Ecowas (kundi la mataifa ya Afrika Magharibi).”

Aidha, aliomba radhi kwa raia, akisema hilo tu ndilo wawezalo kufanya kwa sasa.

Viongozi wa Ecowas wanaopatanisha kwenye mzozo huo wanatarajiwa kukutana tena Nigeria baadaye leo.

Mpango wao unahusisha kurejeshwa kwa serikali ya kiraia, msamaha kwa waliohusika kwenye mapinduzi ya serikali na kufanyika kwa uchaguzi mkuu Novemba.

Unasemaje kuhusu hii?

mrishokafir alisema, tarehe 2015-08-13 09:40:07:
Ni blog kali sana na ni mahiri kwa upakuaji wa ngoma, nawapongeza kwa hilo mmeweza,endeleen kukimbiza around in every where to run de world wide

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
Bookmark and Share
deSiGned by sundo