Pambano la Chris Brown na Soulja Boy kufanyika Dubai
imewekwa na Kibonde
muda 2017-01-11 00:43:39
Watazamaji 261
Pambano la Chris Brown na Soulja Boy kufanyika Dubai

Drama ya pambano la Chris Brown na Soulja Boy inazhttp://www.tabelltz.com/zakimataifaadmin.phpidi kushika kasi. Imedaiwa kuwa pambano la ngumi la wawili hao lipigwa katika ulingo huko Dubai.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa TMZ, wawili hao wamekubali kupigana kwenye pambano hilo ila wanachotaka ni kupata fedha zaidi kupitia kwa watu ambao watataka kuangalia pambano hilo [Pay-Per-View].

Awali pambano hilo lilipangwa kufanyika mjini Las Vegas lakini kutokana na sheria zilizopo katika mji huo kutokana na mapambano kama hayo ndio imesababisha kubadilishwa kwa ratiba hiyo. Hata hivyo imedaiwa kuwa pambano hilo litakuwa ni kwa ajili ya kujitolea na fedha zitakazopatikana zitatolewa kama msaada.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
Bookmark and Share
deSiGned by sundo