Marekani yaendelea na mpango wa kuwahamisha wafungwa toka Guantanamo Bay
imewekwa na Kibonde
muda 2017-01-06 02:59:00
Watazamaji 72
Marekani yaendelea na mpango wa kuwahamisha wafungwa toka Guantanamo Bay

Marekani imewaachia baadhi ya wafungwa wa Yemen waliokuwa wakishikiliwa katika gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba.

Mmoja kati ya wafungwa waliohamishwa kutoka Guantanamo Bay akisalimiana na ndugu zake

Makao makuu ya Pentagon yamethibitisha kuwahamisha wafungwa hao na kusema kuwa kwa sasa ni wafungwa 55 wamebakia katika gereza hilo. Mwandishi wa AFP amedai kuwa aliwaona wafungwa wanne wakishuka katika uwanja wa ndege wa Riyadh ambao umezoeleka kwa kutua viongozi wakubwa.

Baada ya kuwaona ndugu zao mmoja wa ndugu wa wafungwa hao, Mohammed Bawazir alisema, “I want to give back to my family the 15 years I lost.”

Hivi karibuni Marekani iliahidi kuendelea na mpango wake wa kuwahamisha wafungwa waliopo katika gereza la Guantanamo Bay kitendo ambacho kimekuwa kikipingwa vikali na Rais mteule wa nchi hiyo, Donald Trump

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
Bookmark and Share
deSiGned by sundo