YouTube yafunga akaunti ya televisheni ya Korea Kaskazini
imewekwa na admin
muda 2016-12-17 01:16:47
Watazamaji 55
YouTube yafunga akaunti ya televisheni ya Korea Kaskazini

Mtandao wa video wa YouTube umefunga akaunti ya mtandoa huo inayotumiwa na shirika la habari la Televisheni la Korea Kaskazini.Ujumbe unaoonekana kwenye akaunti hiyo unasema kuwa umefungwa kwa kukiuka kanuni za YouTube.

Akaunti hiyo hutumiwa kutangaza matukio ya kila siku.Ripoti zinasema kuwa sababu kuu ya kufungwa akaunti hiyo ni kuwa Korea Kaskazini ilikuw ikipata malipo ya biashara kupitia akaunti hiyo ambayo inaweza kukiuka vikwazo vya Marekani.

Akaunti ya televisheni ya Korean Kaskazini iliyofungwa

akaunti  ya korea kaskazini iliyofungiwa

 

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, akaunti hiyo ilifungwa mwezi uliopita na mtandoa wa Google ili kuzuia kukiuka vikwazo.

Google haitamki lolote kuhusu hatua hiyo lakini hata hivuo imesema kuwa hufunga mitandao ambayo hukiuka kanuni za mtandao wa YouTube wakati inahitajika kufanya hivyo kisheria.Mwezi Januari mtandao huo ulikuwa ukitangaza habari za majario ya mabomu ya nuklia.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
Bookmark and Share
deSiGned by sundo