DIAMOND,VANESSA,ALI KIBA WAPIGWA ‘NGUMI JIWE’ MTV-MAMA2016
imewekwa na mshindi
muda 2016-10-23 03:06:29
Watazamaji 638
DIAMOND,VANESSA,ALI KIBA WAPIGWA ‘NGUMI JIWE’ MTV-MAMA2016
Uko hapa : Home > Habari za mastaa>

Wawakilishi wa Tanzania katika tuzo za wanamuziki bora zinazoandaliwa na MTV Africa Music Awards 2016 (MAMA)  hawakufanikiwa kutwaa tuzo yoyote japokuwa waliweza kushiriki katika vipengele tofauti.

Katika tuzo hizo zilizotolewa Johannesburg, Afrika Kusini kuamkia leo, dalili zilionekana mapema kuwa mbaya kwani Vanessa Mdee aliyekuwa anawania tuzo ya msanii bora wa kike alishindwa baada ya Yemi Alade (Nigeria) kutangazwa mshindi.

mtv-mama-11

Kama hiyo haitoshi, Diamond Platinumz aliyekuwa anashindania tuzo ya msanii bora wa mwaka akipambana vikali na Black Coffee, Sauti Sol, Wizkid na Yemi Alade alishuhudia tuzo hiyo akikabidhiwa Wizkid.

Wimbo “Unconditionally Bae” ulioimbwa na Sauti Sol akishirikiana na Alikiba, ambao ulikuwa kwenye kipengele cha wimbo bora wa kushirikishwa haukupata tuzo. Wimbo huo pia uliambulia patupu katika kipengele cha wimbo bora wa mwaka.

Hata hivyo, Yamoto Band iliyoshiriki katika tuzo hizo katika kipengele cha ‘Chaguo la Wasilikizaji’ haikufanikiwa kutwaa tuzo hiyo.

Msanii mwingine kutoka Tanzania aliyeshiriki tuzo hizo maarufu barani Afrika na kushindwa kufurukuta katika medani hiyo ya kimataifa ni Raymond.

Unasemaje kuhusu hii?

Ama d Rd shy alisema, tarehe 2015-08-07 09:31:43:
Pink ume do wek gud kinoma uwe mwanzo mzur bby

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
Loading...
Bookmark and Share
deSiGned by sundo